TUMEFUNGWA KATIKA MUDA.


Bwana Yesu asifiwe……….

Maisha ya mwanadamu yamfunguwa na MUDA hapa Duniani hatuna mji udumuo Bali tunatazamia mji Wa mwana kondoo mbingu mpya. Hivyo Fanya yote kwa wakati na muda ulionao hapa Duniani. Maana ujana, uzee, au cheo au uhai . una wakati na majira take hapa Duniani. Kuna miaka miaka ya shida na miaka ya heri hapa Duniani. Wewe umeamua maisha ya aina gani?

Hivyo wakati Wa kuoa na kuolewa uwe unafanya hivyo. Pamoja na kazi umayofanya.

(Mwa 47 )
————
8 Farao akamwuliza Yakobo, Je! Siku za miaka ya maisha yako ni ngapi?

9 Yakobo akamjibu Farao, Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni mia na thelathini; siku za miaka ya maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikilia siku za miaka ya maisha ya baba zangu katika siku za kusafiri kwao.

Yakobo hapa anaongea kama MTU mwenye majuto katika uzee wake mbele ya Farao Wa Misri. Kuwa miaka yake imekuwa chache………

1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
Mhubiri 3 :1

2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;
Mhubiri 3 :2

3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
Mhubiri 3 :3

4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;
Mhubiri 3 :4

5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;
Mhubiri 3 :5

6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;
Mhubiri 3 :6

7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;
Mhubiri 3 :7

8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.
Mhubiri 3 :8

9 Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo

HAPA DUNIANI HATUNA MJI UDUMUO.

(Ebr 13 )
————
12 Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango.

13 Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutumu lake.

14 Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.

15 Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.

16 Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.

(1Pe 2 )
————
11 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.

12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.

Advertisements