BWANA NI NGUVU ZANGU


BWANA NI NGUVU ZANGU

Usitegemee NGUVU za pesa, mwili, elimu, cheo, ……BaliπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

*”Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.”*
(Kuto 15: 2)
*”Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.”*
(Zab 28: 7)

: _*”Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu.”*_

(Zab 118: 14)

_*”YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.”*_

(Hab 3: 19)

: bali wao wamngojeao Bwana watapata *_nguvu mpya;_* watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.

Isaya 40:31

*Lakini mtapokea nguvu,* akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Matendo ya Mitume 1:8

*”Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.”*

(Zek 4: 6)

Advertisements