MUNGU AMETUSHIRIKISHA UTUKUFU WAKE


Utukufu ni nini?

Utukufu ni heshima au sifa kuu au ukuu unaojidhirisha katika ya wanadamu. Utukufu katika dhana ya kikristo ni ukuu Wa Mungu unaothihirishwa mbele ya wanadamu…..Hata hivyo hatawezi kueelezea ukuu na sifa za Mungu zilivyo za ajabu sana, ila tutauona utukufu kwa viwango vya juu Siku ile USO kwa USO.

Je!Mungu anaweza kushirikisha utukufu wake kwa wanadamu?

Katika uumbaji Mungu aliweka sehemu ya heshima yake au utukufu wake kwa mwanadamu.

26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mwanzo 1 :26

27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Mwanzo 1 :27

Kama mwanadamu ameumbwa kwa sura ya Mungu, basis ana sura ya Mungu ndani yake, maana tumepewa heshima ya kutawala juu ya kazi ya mikono ya Mungu zilizoko chini ya Jua…..Tukapewa utukufu mkubwa na heshima….wanyama wakapita mbele ya mwanadamu na kuwaita majina.

UDHIHIRISHO WA UTUKUFU WA MUNGU/(manifestation of Glory Of The Living God.)

Mungu alijiweka wazi kwa Mwanadamu akiongea naye kila wakati na kumpa maelekezo ya kutawala naye katika Bustani ya Edeni …..Mwanadamu alikuwa amejaa utukufu Wa Mungu katika maisha yake Bustanini

UTUKUFU WA MUNGU KUMWACHA MWANDAMU

Dhambi ndiyo inayoondoa utukufu Wa Mungu ndani yetu ile sura na mfano Wa Mungu hutoweka mwanadamu akuwa utupu.

9 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
Mwanzo 3 :9
10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
Mwanzo 3 :10
11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?
Mwanzo 3 :11

“kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;”

(rom 3: 23)

Hivyo mwanadamu anapungukiwa na utukufu Wa Mungu kwa sababu ya dhambi, Utukufu Wa Mungu unapijidhihirisha ukiwa katika dhambi unaweza kufhurika…..mfano Miriam Dada ya Mussa, Bar YESU, Anania na Safira. Ndiyo maana Isaya akasema ole wangu maana macho yake yamemeona Bwana….lakini alipata rehema na kusafishwa dhambi.

NAMNA YA KUPOKEA UTUKUFU WA MUNGU KATIKA MAISHA YETU

Kama utukufu Wa Mungu unaweza kutuacha au kutupungua kwa sababu ya dhambi tukitaka tupate utukufu Wa Mungu katika maisha yetu Fanya yafutayo:

TOBA NA UPATANISHO

Toba ni kuacha maisha yanamfanya Mungu kukasirishwa nayo, Kugeuka na kuacha kabisa kisha kuondoa mafarakano kati yetu na Mungu kwa kufanya upstanisho naye. Mungu atarudisha sura yake ndani mwetu.

(rom 3 )
————
23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;

24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;

25 ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho.

“Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.”
(Yoh 15: 3)

OKOKA NA JAZAWA ROHO MTAKATIFU.

Mtu aliyempokea Bwana Yesu na kujazwa Roho Mtakatifu anarudishiwa SURA ya Mungu ndani yao, kama mwanzo. Maana kama kwa Adamu kutenda dhambi tuliuzwa chani ya dhambi, BWANA YESU tumepata uhai na kurufishiwa Sura ya Mungu ndani yetu. (Kolosai 1:13) Ujazwe Roho Mtakatifu ili MUNGU afanye kazi ndani yao na kudhihirisha utukufu wake katika maisha yetu. “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?”
(1Kor 3: 16)

(Ef 1 )
————
13 Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.

14 Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.

AMINI KAZI ZA YESU KISHA FANYA KAZI NAYE, USITIE SHAKA.

Mtu anayeziamini kazi anazofanya Bwana Yesu, yeye naye atafanya kazi hizo, ukiwa kwenye orodha ya wateule Wa Yesu ujue utafanya naye kazi.

“Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye.”
(Yoh 20: 27)

“Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.”

(Yoh 14: 12)

Hata Bwana Yesu hakufanya kazi mwenyewe Bali na Baba yake.

(Yoh 14 )
————
10 Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.
11 Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.
12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.

MAKUHANI WA KIFALME

HUDUMA YA UKUHANI
_mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu._

“`1 Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,
Waebrania 8 :1

2 mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.
Waebrania 8 :2

3 Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa.
Waebrania 8 :3

4 Kama angekuwa juu ya nchi, asingekuwa kuhani; maana wako watoao sadaka kama iagizavyo sheria;
Waebrania 8 :4

5 watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.
Waebrania 8 :5

6 Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora.
Waebrania 8 :6

7 Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili.
Waebrania 8 :7

8 Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya;
Waebrania 8 :8

9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana.
Waebrania 8 :9

10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.
Waebrania 8 :10

11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.
Waebrania 8 :11

12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena.
Waebrania 8 :12

13 Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.
Waebrania 8 :13“`

_massidominick@gmail.com_

Advertisements