ROHO MTAKATIFU AKIJA JUU YAKO NINI KINATOKEA?


ROHO MTAKATIFU AKAJA JUU YAKO NINI KINATOKEA?

35 Malaika akajibu akamwambia,
*Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli;*
kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

ROHO MTAKATIFU ATAKUJILIA JUU YAKO, NA NGUVU ZAKE ALIYE JUU===
๐ŸŽคTunahitaji Roho mtakatifu atufunike kwa nguvu ili kitu cha kimungu kizaliwe.
๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑNeema ya Mungu itakufunika kama kivuli…. Kama Roho Mtakatifu hayupo juu yako roho nyingine itakutesa.
YESU KRISTO MWENYEWE HAKUANZA BILA ROHO MTAKATIFU KUWA JUU YAKE
14 Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.
Luka 4 :14

18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,*
Luka 4 :18
Mathayo : Mlango 3
16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;

UBADILISHWE UWE MTU MWINGINE. UTU KALE UONDOLEWE NDANI YAKO.

1 Wakoritho : Mlango 6
11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.Mtukuze Mungu katika Mwili na Roho*

*SAULI ALIBADILISHWA*
6 na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine.
1 Samweli 10 :6

Kumbuka kuwa ili ufanyike mtoto wa Mungu ni Lazima ujazwe Roho Mtakatifu mtakatifu_
Maana Bwana Yesu kabla ya kupaa kwake aliwaahidi mitume kuwa atawaletea ahadi kutoka kwa Baba.
๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ49 Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.
Luka 24 :49

TUNA AHADI YA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU

Matendo : Mlango 2
*39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.*

๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
*BILA ROHO MTAKATIFU HATUWEZI KITU*
Zakaria : Mlango 4
6 Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi.

Nakutakia baraka za Rohoni kama tulivyoahidiwa na Bwana Yesu Kristo mfalme wetu.
Uwe mtu wa rohoni ili ujue mambo ya rohoni……

๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑmassidominick@gmail.com

Advertisements