UKUAJI KATIKA WOKOVU NI KUJUA NINI?


NAKUOMBEA KWA MUNGU SOMA HII.

“`UKUAJI KATIKA WOKOVU NI KUJUA NINI?

*Kumjua Mungu wa kweli wa pekee.*
Mungu wetu hafananishiwi na kitu chochote hapa duniani, mbinguni na hata chini ya nchi.
Hairuhusu sisi tuabudu vitu au kuiheshimu au kuvitumikia au kuiheshimu.
Yeye asiyefananishwa na kazi ya mikono ya binadamu….
Mfano katika baadhi ya dini wanasema TUWAHESHIMU… Lakini kwa Mungu ni chukizo…
“`Matendo17

25 wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.
1 Mungu akanena maneno haya yote akasema,
Kutoka 20 :1

2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
Kutoka 20 :2

3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
Kutoka 20 :3

4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
Kutoka 20 :4

5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Kutoka 20 :5

“`

*Upate walimu sahihi wa Neno la Mungu*

Ili TUSIPOTIE mbali na kweli ya Mungu lazima tupate kweli ya Neno sahihi ya Mungu kwa watu sahihi.
Siyo mapokeo ya kibinadamu.
πŸ‘‰kanisa limesafiri miaka 2018
Hapa ni kanisa la Agano jipya la milele ilifanywa na mitume. Lakini kuna desturi za makabila ya Ulaya yamepenya kanisani.
Mfano kuombea wafu, kuomba wazungu waliokufa… Wakati tukiomba babu zetu wanasema ni chukizo kweli ni chukizo kuomba mtu. Kutokana na hayo Petro mtume wa Yesu anasema hivi… 1 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.
1 Petro 2 :1

2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
1 Petro 2 :2

4 Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.
1 Petro 2 :3
“`

MPENDW JINA LA YESU FAHAMU MWOMBEZI PEKEE NA MWOKOZI PEKEE

*🎀MARIA YA MAMA WA YESU ALIMJUA MWOKOZI WAKE NA ALIMWOMBA.*
Luka : 1

47 Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;
13 Hata walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yohana, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo.
Matendo ya Mitume 1 :13

14 Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.
Matendo ya Mitume 1 :14
*MITUME WALIMJUA MWOKOZI WAO*

29 Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote,
Matendo ya Mitume 4 :29

30 ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.
Matendo ya Mitume 4 :30

31 Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.
Matendo ya Mitume 4 :31

*WEWE NA MIMI TUSILOGWE NA MAFUNDISHO YA UWONGO.*

Maombi tunapaswa kumwomba baba yetu wa mbinguni.
8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.
Mathayo 6 :8

9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
Mathayo 6 :9

10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
Mathayo 6 :10

11 Utupe leo riziki yetu.
Mathayo 6 :11

12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Mathayo 6 :12

13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
Mathayo 6 :13

TUNAYE MWOMBEZI ALIYE HAIπŸ‘ˆπŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜
Kuhusu nani anatuombea katika udhaifu wetu
34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
Warumi 8 :34

22 basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.
Waebrania 7 :22

23 Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae;
Waebrania 7 :23

24 bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.
Waebrania 7 :24

25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Waebrania 7 :25

Yohana : Mlango 17

9 Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;

Yohana : Mlango 17

20 Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.

RAFIKI YAKO NIKUPENDAYE PASTOR MASSI

https://dominickfoundation.wordpress.com/

massidominick@gmail.com
πŸ›πŸ›πŸ›πŸ›πŸ›πŸ›
Shirikisho wengine

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.