KUSIFU NA KUABUDU


Kusifu na kuabudu ni matendo yote ambayo hupewa Mungu mkuu anayeishi milele yote 1nyakati20:22, Yohana 4:22-

KUSIFU 

Kusifu ni neno lilitokana sifa yaani kutukuza na kutaja matendo ya mwenye nguvu juu ya yote, Mungu mkuu anayeweza kufanya mambo ya ajabu kama vile kuponya, kuokoa kuinua viwete, kufufua, mwenye uwezo juu ya Mbingu na dunia.Tunapoona watu wanawasifu wanadamu wenzao na wanaosifiwa wanajisikia vizuri. Hii ni kwa sababu mwanadamu aliumbwa kwa sura ya Mungu. 

Mwanzo1:26 Mungu akasema,Natumfanye mtu kwa sura na mfano wetu; Wakatawale samaki wa baharini,na ndenge wa angani na wanyama, na nchi pia, na kila chenye kutambaa kitaambapo juu ya nchi.  Hivyo tunaposefiwa na watu tujisahau tukapokea sifa na utukiufu bali tumpe Mungu baba aliyetuumba sisi sote. Mpendwa msomaji ni vema kumsifu Muumba wetu kwa nyimbo, maneno na matendo yetu.

 Nyimbo ni njia ya kuwasilisha ujumbe kwa njia ya uimbaji, tunapaswa tumwimbie Mungu nyimbo za sifa katika ibada zetu. Mara nyingi watu wanapuuza kusifu na kufanya watu, kujiburudisha kwa pambio na kukata viuno kitu ambacho si kusudi la Mungu kutupa nafasi ya kuishi duniani. Zaburi22:3 Na wewe u mtakatifu, juu ya sifa za Israel. Mungu anaketi juu ya sifa za watu wake, hii ina maanisha kama tukimsifu Mungu tunaandaa mazingira ya Mungu kushuka kwetu na kujidhirisha kwetu. Hivyo nyimbo, matendo ya kucheze kwa heshima katika Ibada inamfanya Mungu atupe kibali.

Swali:

 je! Tunaposifu Mungu yupo?  

Jibu:

Mungu anakuwepo pale pale anaposifiwa. Mfano wakati Daudi alipomsifu Mungu mbele ya sanduku takatifu Mungu alikuwepo. 2samwel 6:5- Daudi alipokuwa anacheza nakumwimbia Mungu mambo haya yalitokea. 

  1. Mungu alimfurikia Uza aliyetaka kumsaidia Mungu asianguke
  2. Daudi aliogopa akaacha kuipeleka sanduku katika mji wa Daudi, bali aliicha katika Nyumba ya mtu moja anaitwa Abed-edomu kwa muda wa miezu mitatu. Mungu akambariki.
  3. Daudi alipoamua kuchukua sanduku alicheza na kuimba nyimbo; lakini Mikali binti Sauli, Mke wa Daudi alikejeli kitendo cha sifa. Mungu akampiga kwa utasa. 

Hivyo nawasihi waimbaji na Wachungaji mpeni Mungu nafasi ya kusifiwa katika kusanyiko lote. Ukisoma zaburi yote inataja habari za kumsifu Mungu. Hizi litrujia za kidini ni mapokeo ya wanadamu tu.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUSIFU

  1. Takatifu.  1nyakati 16:29 Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Leteni sadaka , mje mbele zake; mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.          Kwa safi katika ibada ya kusifu na maisha ya kila siku. 
  2. Unyofu wa moyo. Zaburi 33:1 Mpigieni Bwana vigelegele,enye weye haki, kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo
  3. Kuiweka nafsi yako wazi mbele za Bwana.  Zaburi 42:4 Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani ndani yangu,jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano,Nakuwaongoza nyumbani kwa Mungu, kwa sauti ya furaha na kusifu,mkutano wa sikukuu. 
  4. Kwenda kuhuduria mbele za Bwana. Zabauri43:4 Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu,  kwa Mungu aliyefuraha yangu na shangwe yangu; Ee Mungu, wangu. 

Ingia kwa malangoni mweke kwa kushukuru; nyuani mwake kwa kusifu;mshukuruni, lihimidini jina lake.Zabari 100 Mpendwa msomaji mara nyingi watu hupuuza nafasi ya sifa na kuwaachia vijana. Lakini wachungaji niwaombe sana kuwa tuandae nafasi wa watu kumsifu Mungu. 

     

KUABUDU

Kuabudu ni neno linalotokana na ibada. Ibada ni matendo yote yanayohusisha Kumtukuza Mungu wa mbinguni. Pia wako wanaodanganyika na kuabudu viumbe,miti, mawe na mizimu hao wamedanganyika na shetani. YESU Ametueleza namna ya kumtolea Mungu ibada halisi na kweli inayompendeza. Yohana 4:22-24 Waabuduo halisi wanamwabudu katika Roho na kweli, Yaani utu wa mwoyoni kwa Mungu ya kweli kumtolea Mungu dhabihi na sadaka kumtole Mungu akiyentakatifu ibada. 

Zaburi96:9 Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake. Mwabuduni kwa uzuri wa utakatifu. Hivyo Matendo ya kuabudu yanakamilika kwa moyo safi na utakatifu kwa kumwabudu katiks Roho na kweli.  IBADA iliyo ya moyo safi kama ya Abel mwanzo 4:1-2

Mungu awabariki kwa kusoma kwenu. By

Pastor Dominick massi

Unaweza kunipata kwenye mtandao kwa 

Pastor Dominick foundation htts://dominickfoundation.wordpress.com.

Email:massidominick@gmail.com

Facebook:Dominick massi.

BarikiweAdvertisements