KUZALIWA MARA YA PILI


UTANGULIZI:

Kuzaliwa mara ya pili inatokana na dhana kwamba mtu anazaliwa mara ya kwanza kwa jinsi ya mwili.(mtoto). Dhana ya pili ni kuzaliwa kiroho katika ufalme wa Mungu. Katika makala hii tutazungumzia dhana ya kuzaliwa mara ya pili kiroho na wala si kwajinsi ya mwili. Kabla ya kuelezea vizuri kufafanua dhana hizi mbili kama ifuatavyo:

KUZALIWA KIMWILI
Mtoto huzaliwa katika mwili, kutoka katika ukoo fulani na anakuwa ndugu katika familia ya ukoo fulani. Hebu tuchunguze Biblia takatifu; Mathayo1:1-23 tunaona kwa kufuata mpango wa Mungu,Yesu alizaliwa kwa jinsi ya mwili kutoka kwa ukoo wa Ibrahimu aliye baba wa Imani. Hivyo hata mimi na wewe tumezaliwa na wazazi wetu na tunapaswa tuwatii katika BWANA. Luka 2:51,52

.
KUZALIWA MARA YA PILI
Kuzaliwa mara ya pili, ni kitendo cha mtu kubadilisha maamuzi yake ya ndani na kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wako. Hii hutokea kwa wale wenyenyekevu wa moyo Yohana 3:1-12 Bwana Yesu alizungumza na mwalimu wa sheria,Nikodemu kwa habari ya kuzaliwa mara ya pili; Yesu alilimhimiza kuwa ni lazima kuzaliwa mara ya pili ili uingie katika ufalme wa Mungu. Kuzaliwa mara ya pili ni kuwa kiumbe kipya katika utu wa ndani, yaani utu wa moyoni na kuondolewa utu wako wa kale ambao haumpendezi Mungu. Katika lugha ya Biblia mtu wa kale ni mtu wa asili 1korintho 2:14“Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo Roho wa Mungu: maana kwake huyo ni upuuzi,wala hawezi kuyafahamu, kwakuwa hutambulukana kwa jinsi ya rohoni.” Hivyo Yesu akiingia ndani ya moyo wako kupitia Neno lake unalohubiriwa kwa kuiamini na kupokea basi utazaliwa mara ya pili. Hilo litakufanya uchukie dhambi na kupenda haki maana Roho wa Mungu atakuwa ndani yako. 2korintho 5:17. Hata mtu imekuwa mtu akiwa ndani ya Yesu amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. Galatia 6:15“Kwa sababu kutahiriwa si kitu bali kiumbe kipya” Mpendwa msomaji wangu NEEMA ya Mungu yatotosha kubalisha maisha yetu na kutufanya kuwa wana wa Mungu wasio na hatia mbele zake maana waliompokea hufanyika watoto wa MUNGU. Yohana 1:12. Wale wanaompokea Yesu wanapata furusa ya kuwa wana wa MUNGU. Hivyo hakuna haja ya kuishi nje ya Neema hii amboyo Yesu ametupatia ana mwisho wake.2korintho6:1-2. Ni vema kutumia fursa hii vema maana baada ya kufu hutaipata Ebrania 9: 27
UBARIKIWE. IMEANDALIWA NA PASTOR DOMINICK MASSI

Advertisements